| Lango la shule ya uanasheria |
Kaimu naibu mkuu wa chuo kikuu cha Moi mjini Eldoret amekana madai kwamba chuo hicho hakijaidhinishwa kutoa mafunzo ya uanasheria nchini. Profesa Laban Ayiro alisema haya kwenye hafla ya kufuzu kwa mahafali elfu 4,690 katika chuo hicho.
Vilevile alidokeza kuwa usimamizi wa chuo hicho umeiomba wizara ya elimu kukagua wahadhiri wake na maktaba ya chuo hicho wakishikilia kwamba masuala yote yamezingatiwa na chuo hicho katika kutoa mafunzo ya uana sharia
Aidha viongozi wa kaunti ya Uasin Gishu wameitaka serikali kuongeza ufadhili kwa chuo kikuu cha Moi. Naibu gavana Daniel Chemno amesema licha ya chuo hicho kukuza viongozi tajika katika sekta mbalimbali hadhi yake imeshuka pakubwa kutokana na uhaba wa fedha
No comments:
Post a Comment