Wanafunzi wa kike wamegonga tena vichwa vya habari kwa kudhihirisha umahiri wao katika masomo na kuwashinda wenzao wa kiume mwaka huu katika mtihani wa kidato cha nne KCSE
Karimi Naomi Wawira wa shule ya upili ya wasichana ya pangani alipata alama 87.11 huku akiibuka wa kwanza nchini, Sharon Chepchumba kutoka shule ya upili ya wasichana ya Moi mjini Eldoret na Brian Maina wa shule ya wavulana ya alliance wakipata alama 86.757 huku wakichukua nafasi ya pili na ya tatu mtawalia
Odero Donata wa shule ya Lenana alichukuwa nafasi ya nne naye Harriet Mueke kutoka Mary Hill akiwa wa tano
| Picha ya wanafunzi wakisherehekea |
Akizungumza wakati wa kutoa matokeo waziri Matiang'i alizipongeza shulu za wasichana kwa kufanya vyema kuliko za wavulana
Wanafunzi 142 walipata alama za A ikilinganishwa na mwaka jana ambapo ni wanafunzi 141 pekee waliopata alama ya A. Vilevile idadi ya wanafunzi waliopata alama ya A hasi imepungua kutoka elfu 4,645 mwaka wa elfu 2016 hadi elfu 2,714 mwaka wa 2017

No comments:
Post a Comment