| Magari yaliohusika katika ajali |
Saba hao walikumbana na mauti walipokuwa njiani wakielekea kwenye matanga. Kamishna wa kaunti ya Makueni Mohammed Maalim amedhibitisha ajali hiyo akielezea kuwa dereva wa gari hilo lililokuwa limebeba waombolezaji lilikuwa linajaribu kulipita gari lilipogongana na lori lililokuwa likielekea Nairobi kutoka Mombasa.
Takriban watu 180 wamepoteza maisha yao kutokana na ajali ya barabara tangu mwezi disemba ulipoanza huku sababu kuu za ajali hizo kutokea zikiwa kuendesha gari kwa kasi, uendeshaji gari wakati dereva amelewa na kadhalika
Siku ya Jumanne disemba 19 serikali kupitia halmashauri ya usalama barabarani NTSA ilitoa orodha mpya ya hatua zitakazochukuliwa dhidi ya madereva watakaovunja sheria hizo hii ikiwa njia moja wapo tu ya kupunguza ajali barabarani .



