Tuesday, 16 January 2018

RAIS AKUTANA NA WAWAKILISHI WA EALA

Rais Uhuru Kenyatta alikutana na wabunge waliochaguliwa kuiwakilisha kenya katika bunge la EALA siku ya Jumatatu(15 Januari 2018) na kuwasihi kuyapa maswala yanayohusu kenya kipao mbele wanapofanyakazi ili kuleta utangamano baina ya mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki. Wabunge hao Simon Mbugua,Kennedy Kalonzo,Fatuma Ibrahim,Wanjiku Muhia,Nooru Adan, Florence Jematiah, Mpuri Apuri na Abdikadir Omar Aden walichukuwa nafasi za afisi takriban wiki tatu zilizopita. Rais vilevile aliwaomba kuhakikisha kuwa tofauti zao za kisiasa haziathiri utendakazi wao katika bunge hilo

Aidha rais aliwaahidi kufanya kazi kwa karibu na hata kufanya mikutano kila mara ili kuhakikisha kuwa wajibu wao katika bunge hilo linakuwa la manufaa kwa wakenya na hata wakaazi wa Afrika Mashariki Waliohudhuriaa mkutano hua pia ni kiongozi wa wengi katika bunge Aden Duale na waziri wa Leba na Maswala ya Jumuia yaAfrika Mashariki Phylis Kandie.

Saturday, 6 January 2018

RAIS AWATEMA MAWAZIRI 13

Mawaziri kumi na watatu wakiwemo Amina Mohamed (Mashauri ya kigeni), Aden Mohamed (Viwanda),Raychelle Omamo (Ulinzi),Eugine Wamalwa (Maji), Judy Wakhungu(Mazingira),Phylis Kandie(Leba na maswala ya Jumuia ya Afrika Mashariki),Cleophas Mailu(Afya), Mwangi Kiunjuri(Ugatuzi),Dan Kazungu(Madini),Hassan Wario(Michezo),Jacob Kaimenyi(Ardhi),Willy Bett(Kilimo), na Sicily Kariuki(Shughuliza utendakazi wa umma, vijana na jinsia ) waliokuwa wakihudumu katika baraza la mawaziri la Rais Uhuru Kenyatta wametemwa huku sita wakisalia Katika jumla ya mawaziri kumi na tisa waliohudumu katika awamu ya kwanza.

Rais hata hivyo anatarajiwa kutoa orodha kamili ya watakaochukuwa nafasi tofauti katika baraza lake jipya la mawaziri katika awamu yake ya pili na ya mwisho wiki ijayo.

Monday, 1 January 2018

INTERACTIVE CORNER: ILANI YA NTSA YAATHIRI UCHUKUZI NCHINI

INTERACTIVE CORNER: ILANI YA NTSA YAATHIRI UCHUKUZI NCHINI: Abiria wengi waliokuwa wanatarajia kusafiri usiku wa kuamkia siku ya Jumatatu wameathirika pakubwa kutokana na marufuku ya serikali na maml...

ILANI YA NTSA YAATHIRI UCHUKUZI NCHINI

Abiria wengi waliokuwa wanatarajia kusafiri usiku wa kuamkia siku ya Jumatatu wameathirika pakubwa kutokana na marufuku ya serikali na mamlaka ya usalama barabarani NTSA kusitisha usafiri wa usiku.
Hatua hiyo imejiri kufuatia ajali mbaya iliyotokea eneo la migaa kaunti ya Narok ambapo watu 36 waliaga dunia siku ya Jumapili, huku ikichangia nauli kupanda mara dufu katika baadhi ya maeneo nchini.
Image result for PICTURE OF TRAVELLERS WHO ARE STRANDED IN KENYA DURING THE FESTIVE SEASON
Abiria wapiga kambi kwenye vituo vya mabasi

Baadhi ya kampuni za mabasi za kubeba abiria wanaotoka Mombasa wakija jijini Nairobi zimeongeza nauli hadi shilingi elfu mbili (2000) kiwango ambacho ni cha juu sana ikilinganishwa na ile ya kawaida ambayo ni elfu moja(1000).Hali sawa na hiyo imeshuhudiwa katika vituo vya mabasi mjini kitale kaunti  ya Trans-nzoia huku baadhi ya abiria wakilalamikia marufuku hiyo wakisema hatua hiyo imekuwa ya ghafla  na ya kutokuwa na suluhu kwa tatizo la ajali barabarani

Mwenyekiti wa baraza la magavana Jospahat Nanok amesema ni sharti NTSA ishirikiane na halmashauri ya ujenzi barabara kuu ili kutafuta suluhu ya ajali hizo. Nanok vilevile amesema ni jambo la kusikitisha kwa wakenya wengi kuaga dunia kufuatia ajali zinazoweza kuepukika

FORGET ABOUT 2017, 2018 IS HERE!!

Its a new dawn, new year, new beginning,new season a year to forget the past and all the hurdles that you went through . Last year was a year that was defined and shaped with long electioneering period that has never been experienced in our country. Tragic accidents were the order of the day the killer roads claiming at least 200 lives of people.

Now all is gone, though still fresh in our minds,its now time to focus on the positive and not the negative. We now have to proclaim a year of success and happiness not that of sadness. Though challenges will be there because every new thing comes with its challenges and obstacle but we have to maneuver.
All we need is courage, hope,faith and trust in God to overcome all the hurdles that we may face or come our way. May God grant us all that which our heart desires, may our goals and targets we set come to pass; be it business goal,education goals and relationship. Let it be a year of revolution to all

"The new year stands before you like a blank chapter in a book that has to be written on"